"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.
Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.
Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".
Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.
Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.
Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.
Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.
Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?
Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.
Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.
Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.
Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".
7 Februari 2008
Bungeni, Dodoma.
Tanzania History
Jumatatu, 6 Februari 2017
Tanzania History: Edward Lowassa ajiuzulu

Alhamisi, 26 Januari 2017
Tanzania History: Timu ya Soka ya Tanzania yaigaragaza Marekani.
KWA watu wengi waliofika ngazi ya elimu ya sekondari, jina Richard Mabala linapotajwa, jambo la kwanza watalolikumbuka ni vitabu vyake maarufu vya fasihi vya “Mabala The Farmer” na “Hawa the Bus Driver”. Wengine watamkumbuka kwa mashairi yake ya Kiingereza yaliyomo kwenye vitabu vya “Summons: Poems From Tanzania” na “Selected Poems”.
Richard Mabala ni mtu wa namna gani hasa? Kwenye makala haya tunakuletea mambo 10 ambayo pengine ulikuwa huyajui kuhusu Richard Mabala, mwandishi maarufu wa vitabu, mwanafasihi, mkereketwa wa elimu ya Tanzania, mhamasishaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia nchini, mwanasafu kwenye magazeti mbalimbali na mwanaharakati kupitia Asasi ya TAMASHA. Mambo hayo ni yafuatayo:
1. MNYAMWEZI MKOROGO!
Jambo moja ambalo baadhi ya wasomaji wa vitabu na makala zake wanaweza wasilijue kuhusu yeye, hasa kutokana na anavyokimudu Kiswahili kwa uweledi wa hali ya juu, ni kwamba Richard Mabala ni mzungu. Richard Mabala alikuja nchini mwaka 1973 akiwa miongoni mwa Wafanyakazi wa kujitolea chini ya mpango wa Wafanyakazi wa kujitolea (Voluntary Service Oversea-VSO).
Chini ya VSO, utaratibu ulikuwa Wafanyakazi kutoka uingereza walikuwa wanalipwa mshahara ule ule waliokuwa wanalipwa Wafanyakazi wa Tanzania. Mabala ambaye amewahi kufanya kazi kwa muda mrefu mkoani Tabora hupenda kujiita kwa jina la utani la ‘’Mnyamwezi Mkorogo’’.
2. TOKA RICHARD SATTERTHWAITE HADI RICHARD MABALA
Alipofika Tanzania, Richard Mabala anasema jina lake la asili lilikuwa ni Richard Satterthwaite. Kutokana na kuwawia vigumu wenyeji kulitamka jina hilo, aliamua kubadili jina na kujiita Mabala. Jina hilo Mabala limetoka wapi? Mwenyewe anasema, “Nilijiunga na kwaya ya Ipuli kule Tabora, mwishoni na baada ya kuzoeana wanakwaya wenzangu walisema kuwa hawawezi kulitamka jina langu na kwamba watanipa la kwao; Mabala. Nilipowauliza lina maana gani wakasema ‘eneo kubwa la nje’ kutoka Uingereza hadi Tabora. Kwa kweli nilianza kulitumia jina hili kwa wasiwasi kidogo nikiona watu wanaweza kuniona najitia kimbelembele kulia kuliko mfiwa, lakini kila mtu akalipenda. Kwa hiyo baada ya kunogewa na kupata uraia nikaliongeza na kuwa jina rasmi”.
3. URAIA NA FAHARI YA UTANZANIA
Baada ya kuvutiwa na Tanzania, Mabala alikata shauri kuwa raia kamili wa nchi hii adhwimu. Harakati zake za kusaka Uraia alizianza rasmi mwaka 1979 ambapo Richard Mabala alipeleka maombi ya uraia kwa mamlaka zinazohusika na hilo, maombi yake hayo yakaridhiwa miaka miwili baadaye na akawa Mtanzania kamili. Mabala anasema kuwa hajawahi kamwe kujutia uamuzi wake wa kubadili uraia licha ya kulazimika kupitia mlolongo mrefu wa kuomba Viza kila anapotaka kwenda kumjulia hali mama mzazi yake aliyeko Uingereza.
Mabala anasema kamwe rangi yake haijawahi kuwa kikwazo katika utekelezaji wa shughuli zake mbalimbali hapa nchini.
4. MWALIMU WA MA-NGULI
Kwa vipindi tofauti Mabala amefundisha kwenye shule na vyuo mbalimbali nchini. Baadhi ya shule na vyuo alivyofundisha ni Mirambo, Mzumbe, Korogwe, vyuo vya ualimu Chang’ombe na Marangu. Pia amewahi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Mabala analikumbuka zaidi darasa lake la kwanza la Shule ya sekondari ya Wavulana Mirambo ambalo lilikuwa na wanafunzi ambao sasa ni wanasiasa na wanazuoni nguli.
Baadhi yao ni Marehemu Profesa Jwani Mwaikusa, Mwanazuoni wa Sheria aliyebobea na Wakili katika Mahakama ya Kimataifa Maalum ya Mashtaka ya Jinai juu ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, ICTR, iliyoko Arusha, Profesa Abdallah Njozi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro na Mwanafasihi Mbobezi wa Lugha ya Kingereza na Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi.
5. MWALIMU MSIKIVU
Baada ya Uhuru, uchapishaji wa vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili ulishika kasi. Uchapishaji wa vitabu kwa lugha ya Kiingereza hasa vile vya fasihi vilivyoandikwa na waandishi wa kitanzania ulidorora. Kitabu cha ‘’Summons: Poem from Tanzania’’ kilikuwa kati ya diwani za mwanzo kabisa za ushairi wa Kiingereza kuchapishwa nchini baada ya uhuru. Kazi hii ambayo inajumuisha mashairi ya waandishi mbalimbali wa Kitanzania kama Kajubi Mukajanga, Isaac Mruma, Kundi Faraja, Jwani Mwaikusa na Mabala mwenyewe ilikuwa ni zao la ushirikiano wa Mabala na waliokuwa wanafunzi wake wa sekondari. Mabala anasema kuwa wanafunzi wake walikuwa wakimpatia changamoto ya kuandika kazi zake mwenyewe badala ya kuishia kuchambua na kuzikosoa kazi za wengine.
Mabala anasema “Kajubi Mukajanga (ambaye sasa ni Katibu wa Baraza la Habari-MCT) ndiye aliyenishawishi kuandika mashairi wakati yeye alikuwa mwanafunzi na mimi nilikuwa mwalimu wake. Eti kazi yangu ilikuwa kukosoa wengine kwa nini na mimi nisiandike ili nao wapate nafasi ya kunikosoa”.
Mabala aliifanyia kazi rai ya wanafunzi wake na kuandika mashairi na vitabu vingine vya hadithi.
6. KUTOKA UHADHIRI HADI MWANAHARAKATI
Baada ya miaka mingi ya ualimu, Mabala aliamua kujikita kwenye harakati za Asasi za Kiraia (AZAKI). Yeye ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa AZAKI maarufu kama Haki Elimu na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na mwishowe kwa kushirikiana na vijana, akaanzisha asasi ya TAMASHA yenye makao makuu jijini Arusha.
Mabala anasema “Nillifundisha Milambo, Mzumbe, Chang’ombe TTC, Marangu TTC, Kibosho Girls na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kisha nikatambua kwamba mimi ni mwanaharakati kuliko mwanataaluma (mhadhiri) ndiyo maana nikaingia AZAKI kwa lengo la kuwawezesha vijana. Nimeanzisha TAMASHA (Taasisi ya Maendeleo Shirikishi) tukihimiza vijana wapate nafasi yao katika jamii”
Kati ya mwaka 1999 hadi 2007 Mabala alifanya kazi kwenye shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) kwenye programu ya kuwakomboa vijana wasio shuleni. Mabala alifanya kazi na Unicef kama mwandishi wa mfululizo wa vitabu vya Sara ambavyo vilitafsiriwa kwa Kiswahili. Vitabu vilivyowahi kutolewa katika mfululizo huo ni pamoja na “The Special Gift’’ (Zawadi Maalum), “Daughter of Lioness” (Binti Simba), “The Empty Compound’’ na “Who is the Thief?’’
7. SAUTI YA VIJANA
Vitabu vingi vya Mabala vinahusu watoto na vijana. Mabala anasema kuwa watoto ni kundi lililosahauliwa. Anasisitiza kuwa kamwe haiwezekani kujenga utamaduni wa kupenda kujisomea vitabu kama jitihada hazielekezwi kwa watoto wadogo kwa sababu ni vigumu kuwa na ari ya kupenda kujisomea wakiwa ukubwani.
8. MTETEZI WA KISWAHILI.
Licha ya kuwa kazi zake nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza, Mabala ni miongoni mwa watu wanaopigia chapuo kutumika kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu. Mabala anasema “Kama mwalimu moyo unaumia sana kuingia darasani siku ambayo wanafunzi wamebahatika kupata mwalimu na kukuta sura zilizofadhaika maana hawaelewi wanachofundishwa. Au fanya jaribio la kufundisha kwa Kiingereza lakini uwape kazi ya kujadili katika vikundi. Angalia watakavyochangamkia mada na kujadili kwa kina kwa kiswahili lakini huku wakitumia neno la Kiingereza hapa na pale hasa ya istilahi na wataelewana vizuri sana.”
Mabala anaongeza juu ya hayo kwa kusema, “Msingi wa elimu ni ubunifu na uelewa ndiyo maana nchi zilizo nyingi sana duniani wanahakikisha kwamba wanafundisha watoto wao kwa lugha wanayoielewa. Waholanzi, Waswidi na wengineo wana uwezo wa kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia lakini hawafanyi hivyo maana wanajua kwamba msingi wa elimu na ubunifu, ni uelewa. Na wanajua pia kwamba mara nyingi wanasayansi ndio wabovu kabisa katika kujifunza lugha”.
Kisha anaendelea kusema kuwa “Iwapo tunatengeneza mazingira yanayofaa watoto wetu wanaweza kujua Kiingereza vizuri sana pamoja na kuwa na uelewa wa mambo yote muhimu katika elimu. Mimi nilikuwa sijui Kihispania kabisa lakini kwa muda wa miaka miwili tu, ndani ya shule tu, niliweza kupata 'B' katika A Level. Kwa sababu ya ufundishaji vizuri, mipango makini na pia juhudi yangu. Kwa hiyo hakuna linaloshindikana. Elimu kwanza si lugha kwanza.”
9.BWANA MAKENGEZA NA MWANDISHI WA AYA
Ili kufikisha ujumbe kwa mtindo wa kipekee, Mabala anaendesha safu mbili kwenye magazeti ya Mwananchi (Bwana Makengeza) na Raia Mwema (Aya za Ayah Binti Hidaya). Makala hizo, licha ya kuwasilishwa kwa mtindo wa ucheshi, zimebeba ujumbe mkubwa sana wa hali halisi kwenye jamii. Mathalani, kwenye safu yake ya ‘’Aya za Ayah Binti Hidaya’’, anamtumia mhusika wake mkuu Hidaya ambaye ni mtumishi kwenye nyumba ya Waziri (Waziri wa Mikiki na Makeke) kuonyesha maovu na ghiliba zinazofanywa na wanasiasa.
10. MWANDISHI WA USIKU
Mabala anasema uwingi wa shughuli za Asasi za Kiraia na zile za uandishi kamwe haujawahi kumletea matatizo kwenye familia kwa sababu mkewe anamuunga mkono kwenye kazi zake.’’Mke wangu ni muelewa sana kwa sababu kazi zangu za kuandika nazifanya kati ya saa tisa usiku na saa kumi na mbili asubuhi. Ananiunga mkono sana isipokuwa pale kitanda kinapokuwa cha baridi sana ‘’ anasema Mabala kwa utani.
Pichani ni Mwalimu Richard Mabala (katikati mwenye miwani) akiwa na Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Mirambo mwaka 1974. Kwa maelezo ya Mabala kwenye picha hii ‘’kuna angalau profesa mmoja wa UCLAS, 2 wa UDSM (mmoja marehemu) wakubwa wa BRELA na SUMATRA, generali 1, waziri 1 waandishi maarufu angalau 2 (1 marehemu), kiongozi wa usalama wa taifa. Aidha kuna mkubwa wa bandarini.’’ Unamtambua nani kati yao?
Makala hii iliwahi kuchapishwa kwenye gazeti la SURA YA MTANZANIA ambalo hutoka kila Jumanne.
Shukrani za pekee ziende kwa Ado Shaibu

Jumapili, 26 Juni 2016
Rais John Magufuli afanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuwateua Wakuu wa Wilaya 139
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
Longido - Daniel Geofrey Chongolo
Monduli - Idd Hassan Kimanta
Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
Kinondoni - Ally Hapi
Ilala - Sophia Mjema
Temeke - Felix Jackson Lyaviva
Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
Dodoma - Christina Solomon Mndeme
Chemba - Simon Ezekiel Odunga
Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
Bahi - Elizabeth Simon
Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
Bukombe - Josephat Maganga
Mbogwe - Matha John Mkupasi
Nyang'wale - Hamim Buzohera Gwiyama
Geita - Herman C. Kipufi
Chato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
Mufindi - Jamhuri David William
Kilolo - Asia Juma Abdallah
Iringa - Richard Kasesela
KAGERA
Biharamulo - Saada Abraham Mallunde
Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
Muleba - Richard Henry Ruyango
Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
Ngara - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
Mlele - Rachiel Stephano Kasanda
Mpanda - Lilian Charles Matinga
Tanganyika - Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
Kigoma - Samsoni Renard Anga
Kasulu - Col. Martin Elia Mkisi
Kakonko - Col. Hosea Malonda Ndagala
Uvinza - Mwanamvua Hoza Mlindoko
Buhigwe - Col. Elisha Marco Gagisti
Kibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
Siha - Onesmo Buswelu
Moshi - Kippi Warioba
Mwanga - Aaron Yeseya Mmbago
Rombo - Fatma Hassan Toufiq
Hai - Gelasius Byakanwa
Same - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
Nachingwea - Rukia Akhibu Muwango
Ruangwa - Joseph Joseph Mkirikiti
Liwale - Sarah Vicent Chiwamba
Lindi - Shaibu Issa Ndemanga
Kilwa - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
Babati - Raymond H. Mushi
Mbulu - Chelestion Simba M. Mofungu
Hanang' - Sara Msafiri Ally
Kiteto - Tumaini Benson Magessa
Simanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
Rorya - Simon K. Chacha
Serengeti - Emile Yotham Ntakamulenga
Bunda - Lydia Simeon Bupilipili
Butiama - Anarose Nyamubi
Tarime - Glodious Benard Luoga
Musoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
Chunya - Rehema Manase Madusa
Kyela - Claudia Undalusyege Kitta
Mbeya - William Ntinika Paul
Rungwe - Chalya Julius Nyangidu
Mbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
Gairo - Siriel Shaid Mchembe
Kilombero - James Mugendi Ihunyo
Mvomero - Mohamed Mussa Utali
Morogoro - Regina Reginald Chonjo
Ulanga - Kassema Jacob Joseph
Kilosa - Adam Idd Mgoyi
Malinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
Newala - Aziza Ally Mangosongo
Nanyumbu - Joakim Wangabo
Mtwara - Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
Masasi - Seleman Mzee Seleman
Tandahimba - Sebastian M. Walyuba
MWANZA
Ilemela - Dkt. Leonald Moses Massale
Kwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
Sengerema - Emmanuel Enock Kipole
Nyamagana - Mary Tesha Onesmo
Magu - Hadija Rashid NyemboUkerewe - Estomihn Fransis Chang'ah
Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
Njombe - Ruth Blasio Msafiri
Ludewa - Andrea Axwesso Tsere
Wanging'ombe - Ally Mohamed Kassige
Makete - Veronica Kessy
PWANI
Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed Mwanga
Mkuranga - Filberto H. Sanga
Rufiji - Juma Abdallah Njwayo
Mafia - Shaibu Ahamed Nunduma
Kibaha - Asumpter Nsunju Mshama
Kisarawe - Happyness Seneda William
Kibiti - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface Haule
Nkasi - Said Mohamed Mtanda
Kalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
Namtumbo - Luckness Adrian Amlima
Mbinga - Cosmas Nyano Nshenye
Nyasa - Isabera Octava Chilumba
Tunduru - Juma Homela
Songea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
Kishapu - Nyambonga Daudi Taraba
Kahama - Fadhili Nkulu
Shinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
Busega - Tano Seif Mwera
Maswa - Sefu Abdallah Shekalaghe
Bariadi - Festo Sheimu Kiswaga
Meatu - Joseph Elieza Chilongani
Itilima - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
Mkalama - Jackson Jonas Masako
Manyoni - Mwembe Idephonce Geofrey
Singida - Elias Choro John Tarimo
Ikungi - Fikiri Avias Said
Iramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
Songwe - Samwel JeremiahIleje - Joseph Modest Mkude
Mbozi - Ally Masoud Maswanya
Momba - Juma Said Irando
TABORA
Nzega - Geofrey William Ngudula
Kaliua - Busalama Abel Yeji
Igunga - Mwaipopo John Gabriel
Sikonge - Peres Boniphace Magiri
Tabora - Queen Mwashinga Mlozi
Urambo - Angelina John Kwingwa
Uyui - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
Tanga - Thobias Mwilapwa
Muheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
Mkinga - Yona Lucas Maki
Pangani - Zainab Abdallah Issa
Handeni - Godwin Crydon Gondwe
Korogwe - Robert Gabriel
Kilindi - Sauda Salum Mtondoo
Lushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016
Jumapili, 5 Juni 2016
Bondia MUHAMMAD ALI na Diplomasia ya TANZANIA
Tanzania imekuwa ikifuata sera ya kutofungamana na upande wowote tangu miaka ya 1960 mpaka sasa. Hali hiyo imeifanya Tanzania kuwa na uhusiano na pande zote mbili wakati wa Vita Baridi (Cold War).
Vita Baridi ni mvutano wa kisiasa na kijeshi baina ya Kambi ya Magharibi (Western Bloc) iliyoongozwa na Marekani na Kambi ya Mashariki (Eastern Bloc) iliyoongozwa na Urusi (USSR). Marekani na wenzake walifuata uchumi wa kibepari (capitalist economy) wakati Urusi na washirika wake wakifuata uchumi wa kijamaa (socialist economy). Mvutano huo ulianza mara baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia (WW II) hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Mwaka 1979 Urusi (USSR) iliivamia Afghanistan. Marekani ilipinga vikali kitendo hicho. Wakati huohuo Urusi ilikuwa inafanya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ambayo ilipangwa kufanyika jijini Moscow mwaka unaofuata 1980.
Ili kupata uungwaji mkono kukwamisha michezo hiyo ya olimpiki jijini Moscow mwaka 1980, Marekani ilianza kampeni zake kushawishi baadhi ya nchi zisishiriki mashindano hayo. Katika kujaribu kufanikisha hilo, rais wa Marekani wa wakati huo Jimmy Carter alimtuma bondia MUHAMMAD ALI kutembelea baadhi ya nchi ili aweze kuzishawishi zisusie mashindano hayo maarufu duniani.
Mnamo tarehe 2 Februari 1980 MUHAMMAD ALI aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam (DIA) nchini Tanzania na kulakiwa na Chediel Mgonja, Waziri wa Utamaduni, Vijana na Michezo. MUHAMMAD ALI alipaswa kulakiwa angalau na Waziri wa Mambo ya Nje kwa kuwa ujio wake nchini Tanzania ulikuwa wa kidiplomasia na siyo michezo.
Lengo kuu la bondia huyo lilikuwa kuwasilisha ujumbe wa Rais wa Marekani Jimmy Carter kwa Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Tanzania wakati huo. ALI alitaka amshawishi Mwalimu Julius Nyerere ili Tanzania isishiriki Michezo ya Olimpiki iliyopangwa kufanyika jijini Moscow, Urusi mwaka huo. Pamoja na jitihada nyingi zilizofanywa na maafisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kumshawishi Mwalimu Julius Nyerere kuonana na mwanamasumbwi MUHAMMAD ALI, Mwalimu Nyerere alikataa kabisa ombi hilo.
Baada ya 'bondia mwanadiplomasia' MUHAMMAD ALI kushindwa kuonana na Mwalimu Julius Nyerere, aliamua kuondoka nchini Tanzania na kuelekea nchini Kenya ambapo alilakiwa na Rais Daniel Arap Moi. Kenya ilikubali ushawishi wa Marekani na kususia Michezo ya Olimpiki ya mwaka huo. Tanzania ilikataa ushawishi wa Marekani na kushiriki Michezo ya Olimpiki jijini Moscow, Urusi mwaka huo ambapo ilijinyakulia medali mbili za fedha kupitia wanariadha mashuhuri Suleiman Nyambui na Filbert Bayi.
Diplomasia huhitaji ushawishi. Marekani ilimtumia bondia MUHAMMAD ALI kutokana na umaarufu wake kipindi hicho na pengine kwa kuwa ni Mmarekani mweusi ili nchi za Afrika zishawishike kirahisi. Pia itakumbukwa mwaka 1974 Rais wa Zaire (sasa DRC) Mobutu Seseseko aliandaa mpambano mkali baina ya mabondia wa Marekani MUHAMMAD ALI na George Foreman. Mpambano huo maarufu uliotajwa kuwa "mpambano mkubwa wa karne ya 20" uliofanyika Kinshasa, Zaire na kupewa jina la 'THE RUMBLE IN THE JUNGLE.' ALI alishinda katika mpambano huo kumwongezea umaarufu mkubwa barani Afrika na duniani kote.
Tanzania haikuwa na maslahi yoyote katika uvamizi wa Urusi nchini Afghanistan. Pia Tanzania haikuona sababu yoyote kwanini ikubali ushawishi wa Marekani kususia Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1980. Haya yote yametokana na sera kigeni ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote. Tanzania imekuwa ikifuata sera hiyo tangu miaka ya 1960. Sera hiyo imeifanya Tanzania kuwa na uhusiano na pande zote mbili wakati wa Vita Baridi na hata sasa kama ilivyobainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mhe. Balozi Augustine Mahiga alipowasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2016/2017.
.....................................
Mwandishi wa makala hii ni mwanahistoria na mchambuzi wa masuala ya siasa. Anapatikana kwa barua pepe: tanzaniahistory@yahoo.com
Tupe maoni yako.

Jumatano, 18 Mei 2016
JE, WAJUA? Mlima Kilimanjaro ulikuwa mlima mrefu kuliko yote katika Dola ya Ujerumani (German Empire).
Mlima Kilimanjaro ulikuwa mlima mrefu kuliko yote katika Dola ya Ujerumani (German Empire) hadi mwaka 1918. Dola ya Ujerumani ilijumuisha Ujerumani yenyewe na makoloni yake yote. Baada ya makoloni yake kujinyakulia uhuru, mlima mrefu zaidi uliobaki Ujerumani ya leo ni Mlima Zugspitze wenye urefu wa mita 2,962. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko yote Afrika una urefu wa mita 5,888 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanyika mwaka 2014. Tarehe 5 Oktoba 1889 Mtanzania YOHANA LAUWO akiongozana na Mjerumani HANS MEYER na Muaustria LUDWIG PURTSCHELLER wanakuwa watu wa kwanza kufika kilele cha Kilimanjaro.
Jumatano, 11 Mei 2016
Je, Wajua? Zanzibar iliwahi kuingia katika Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness Duniani.
Mnamo tarehe 17 Januari 1961 Uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria ulifanyika Zanzibar. Afro-Shirazi Party (ASP) ilishinda viti 10, Zanzibar Nationalist Party (ZNP) viti 9 na Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP) viti 3. Zaidi ni kuwa katika jimbo la Chake-Chake ASP ilipata kura 1,538 na ZNP kura 1,537. Hii ni tofauti ya kura moja tu. Katika taarifa ya mwaka ya Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness Duniani (Guinness Book of World Records), matokeo haya yalitajwa kama "matokeo yaliyokaribiana sana."
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)