Jumatano, 18 Mei 2016
JE, WAJUA? Mlima Kilimanjaro ulikuwa mlima mrefu kuliko yote katika Dola ya Ujerumani (German Empire).
Mlima Kilimanjaro ulikuwa mlima mrefu kuliko yote katika Dola ya Ujerumani (German Empire) hadi mwaka 1918. Dola ya Ujerumani ilijumuisha Ujerumani yenyewe na makoloni yake yote. Baada ya makoloni yake kujinyakulia uhuru, mlima mrefu zaidi uliobaki Ujerumani ya leo ni Mlima Zugspitze wenye urefu wa mita 2,962. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko yote Afrika una urefu wa mita 5,888 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanyika mwaka 2014. Tarehe 5 Oktoba 1889 Mtanzania YOHANA LAUWO akiongozana na Mjerumani HANS MEYER na Muaustria LUDWIG PURTSCHELLER wanakuwa watu wa kwanza kufika kilele cha Kilimanjaro.
Jumatano, 11 Mei 2016
Je, Wajua? Zanzibar iliwahi kuingia katika Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness Duniani.
Mnamo tarehe 17 Januari 1961 Uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria ulifanyika Zanzibar. Afro-Shirazi Party (ASP) ilishinda viti 10, Zanzibar Nationalist Party (ZNP) viti 9 na Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP) viti 3. Zaidi ni kuwa katika jimbo la Chake-Chake ASP ilipata kura 1,538 na ZNP kura 1,537. Hii ni tofauti ya kura moja tu. Katika taarifa ya mwaka ya Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness Duniani (Guinness Book of World Records), matokeo haya yalitajwa kama "matokeo yaliyokaribiana sana."
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)