Ota Benga ni binadamu aliyenunuliwa kama mtumwa kutoka Kongo na kuchukuliwa na Wazungu kwenda nchini Marekani katika hifadhi ya wanyama kwa ajili ya maonesho. Mwaka 1904 alishiriki katika 'Maonesho ya Louisiana' ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tangu Marekani iliponunua eneo la Louisiana kutoka kwa Ufaransa. Alikuwa akioneshwa katika maonesho mbalimbali kuelezea hatua za mabadiliko ya binadamu (evolution).
Katika karne ya 20 ilikuwa ni jambo la kawaida binadamu hasa kutoka nchi za Afrika kutumika katika maonesho mbalimbali kuonesha 'hatua za awali' za mabadiliko ya binadamu (early stages of human evolution).
Ota Benga alizaliwa katika Kongo ya Wabelgiji (Belgian Congo) katika jamii ya watu wa Mbuti karibu na Mto Kasai. Aliishi Marekani hadi alipofariki kwa kujiua mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo.
Leo tarehe 20 Machi, 1916 imetimia miaka 100 tangu alipofariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni