Jumamosi, 12 Machi 2016

Diamond Plutnumz amwaga chozi, ni baada ya vipimo vya DNA kuhusu Tifah Dangote

Msanii wa Tanzania Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz na familia yake wamefanya vipimo vya DNA nchini Afrika Kusini na imebainika kuwa Tifah Dangote ni mtoto wao wa kinasaba. Tangu Diamond na Zari Hassan wampate mtoto huyo, kumekuwa na mijadala mingi kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuwa Tifah si mtoto wa Diamond bali mtoto wa Ivan Ssemwanga ambaye ni mume wa zamani wa Zari Hassan. Habari kutoka kwa mtu wa karibu sana na Diamond zinasema nyota huyo wa wimbo 'Utanipenda' inaotamba kwa sasa, alibubujikwa na machozi ya furaha baada ya vipimo kuonesha Tifah ni mtoto wake halali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni