Hivi karibuni nilisoma (mtandaoni) gazeti moja la tarehe 21 Machi 1990 likiwa na kichwa cha habari kinachosema:
"Namibia yapata Uhuru Baada ya Utawala wa Miaka 75 Kutoka Pretoria."
Habari hii ilinikumbusha ujinga wangu zamani. Zamani nilishangaa sana kwanini nchi ya Afrika Kusini inaitawala Namibia ambayo nayo ni nchi ya Afrika. Nilishangaa sana ni kwanini Waafrika wanawaonea kiasi kile Waafrika wenzao.
Baadaye nilikuja kujua kuwa Afrika Kusini ya kipindi kile ilikuwa chini ya utawala wa Makaburu. Makaburu waliitawala Namibia kwa miaka 75 hadi Namibia ilipojinyakulia uhuru wake tarehe 21 Machi 1990.
Hakika bila kufahamu historia, baadhi ya kumbukumbu za kihistoria zitabaki kutushangaza kila siku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni